Hii ni story ya mtaa,
story ya venye si hukaa,
si hua na matime poa
Lakini zile mingi ni mbaya mbaya.
Kuna time mtaani si huona kivumbi
nikaa stress zote kwako ndo zimepiga kambi.
hakuna wode, hakuna stima nguo ziko shabby,
Umesotewa mtu yangu wallet inatoa vumbi,
huna doh ya kunyolewa so nywele iko shaggy,
Kiatu haiwezi kumbuka last time iliona rangi.
Ushaifeel nikaa January hua kila mwezi?
na unahustle daily siati we ni mlazy,
Lakini kusema kwenye pesa yako Huenda joh huwezi,
Hadi unashuku mifuko yako inaeza kuwa na wezi.
Na bado unaonanga watu wana vitambi tao,
eih! Kwani hawa watu hutoa wapi pesa yao?
ju we ukiskia jina landlord we ndo huyooo!!
hutaki akupate nje ya dirisha mbiooo!!!
mwezi ya tatu hujalipa rent na huna kisingizio
Ukipita watoto kwa street unawish ungekuwa mmoja wao
ukiprovidiwa breakfast,lunch na chajio
coz huwezi kumbuka last time kuonja pilau,
eh! Kuku unaona tu kenchic, na ile advert ya Yu.
Mtaani skuhizi hakuna mtu anafford unga,
ona bei ya mafuta pia venye imepanda,
Hadi wezi siku hizi tunachoma na makaa
ju huwezi... huwezi vumilia kuwaste tayaa.
Ooooh, na sikushow hii stuff unihurumie,
nataka upindukie mtaa yenu uiangalie
Halafu ujiulize nini Unaeza ifanyia
Kali
ReplyDeletekama kawa bro ;)...thanks
ReplyDeleteT>R>U>T>H
ReplyDeletethank you :)
ReplyDelete