wanasiasa tuna wachache wazuri
hao wengineni ni wahuni.
wanaduvako na maneno mazuri
kumbe wanatumanga kichinichini.
na maskini bado wanakimbia shoti
wakienda kupewa noti
kisha wanaachwa wakiteta
ati matajiri wanawacheza.
nyi ndo mlijitenda,
mkienda kupewa kimoja
mkaachia mama pima pesa
mkarudi mkiona giza.
keshoye ulevi umeisha
pombe kaisha kwa kichwa,
ndo unaona mashida
karibu upate kichaa.
saizo MP wako ashahinda
yuko parliament anajipanga
vile mshahara atajiongeza
vile ushuru wako ataiba.
sa unaachwa ukilialia
na we nikaa kuku na dua
mwewe ndo huyo ashapaa
na kifaranga wako pia.
ni ten nil amekuchapa
wakidi wamesare chuo wakisaka chapaa
wwanadai chuo wako overshadowed ka Vitz kwa carpark
sa manual labour ndo zao ,vibarua kuchapa
stress nazo zmefanya bibiako akachapa
na venye skuizi ni ngumu kupata mkwanja
ni mafinjefinje,hakuna makapa
unaanza kusaka vibarua
kuchumia chini ya jua
na kivulini hautalia
na home wakidi wanalia
na hauna cha kuwapakulia.
usiku huwezi sinzia
fikra zilivokusumbua
unangoja tena miaka tano
upewe mia na hamsini
uende ulipe madeni
umchague mwingine mhuni.
whatever style you decide to use,you still deliver.Ngartia dear you are good.
ReplyDeletehonestly, I was a bit uneasy about this one :)
ReplyDelete