Nimerealise sauti yangu huwa ndogo kuruka,
nikibonga na watu siezangi skika,
So mi hubonga na pens na mics,
tunadiscuss,
at least hivo, ntajiskia kwa speaker.
Niaje kalamu, Atlast nimekushika
imekuwa siku mob, marraondi tu nikikusaka,
Nimerealise mi hubonga nawewe naishiwa shaka,
najiskia mgwan, ka Zulu Shaka.
So skiza nikushow stuff nliambiwa na Gukaa,
alisema, "Ngartia kwa hii life usiwahi shtuka
hata ile time unaonanga kumethûka,
ile tym bei ya unga haitaki kushuka,
ile tym, sukari haipatikani kwa duka,
karibu uiendee we mwenyewe Kakameka,
ndo time we hushukishiwa baraka
unablessiwa hadi unashtuka.
ju kuku za neighbour kwako ndo zinataga
doggy za mtaa, we ndo zinalinda _
As in ile time kahope kanadidimika,
ndo milango zako zohufunguka."
So Gukaa akapause aeke snuff kwa mapua,
Nikapata îthaa ya kufikiria, kuwaza kuwazua.
nikaona, enyewe, huyu msee ana point mbaya,
Lakini kuagree nayeye ni kitu Siezi fanya,
ju kwa life nimevumilia hadi ile point Siezi vumilia anymore,
Then nikavumilia some more.
Checki, Siezi lipa rent kila mwezi,
Tax kila wakati,
Protection fee kila wiki
ati nalindwa na mungiki,
na naishi kwa shanti!!
Wish ungeona venye nimecladi,
Siezi ng'ara viclassy,
juu ntaattract wezi
wadhani mi ni barbie
Wawe wanakam kwangu daily.
Tuseme jana walibeba telly,
leo wakabeba viti,
Kesho wabebe beddy,
si kesho kutwa ni mabati??
na siati siwajui,
si ni akina mwangi na onyi.
Tuseme hio ni usiku basi,
mchana nachunga hawa polisi,
Ju wanamimina risasi,
nikaa wanalipiza visasi
Wamegeuka ma assassin
wanaua hata makasisi,
je ma hustler ka sisi?
Na bado naambiwa niko free,
Nikiwa citizen wa hii inchi,
na usiku mtaani,
Siezi tembea 9:30,
Mangeta za wagondi.
Mapoliticians hunimanga chini chini,
na wanago scotfree,
Na mimi hapa maskini,
nina dreams za kuwa tajiri,
Ili nieze kuattend poetry event Zenye entrance si free.
No comments:
Post a Comment